Thursday, November 7, 2013

MARTINO AMVULIA KOFIA MESSI.

KOCHA wa klabu ya Barcelona Gerardo Martino amesema Lionel Messi ni mchezaji wa aina yake wakati kikosi chake kilipoisambaratisha AC Milan kwa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Katika mchezo huo Messi alitupia mabao mawili na kuisadia timu yake kuchukua alama zote tatu muhimu na kufuzu hatua ya mtoano katika michuano hiyo. Martino alifurahishwa na nyota huyo wa kimataifa wa Argentina baada ya kupambana kwa muda kurudi katika kiwango chake. Kocha amesema Messi amewafunga midomo wale wote waliokuwa wakimponda katika mchezo huo kwa kuonyesha kiwango chake cha juu. Barcelona itasafiri kuifuata Ajax Amsterdam katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inayofuata kabla ya kumaliza mechi za makundi wa kuikaribisha Celtic nyumbani.

No comments:

Post a Comment