IMEMCHUKUA miaka mingi kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kurudisha ukuta madhubuti aliorithi wakati anaanza kuinoa klabu hiyo Septemba mwaka 1996 na baada ya kuhangaika sana hatimaye ameweza. Iwe kwa bahati mbaya au uamuzi, Wenger hivi sasa ana mabeki wanne vijana wanaocheza kwa uelewano na hawapendi kuruhusu bao ambao ni Per Mertesacker, Laurent Koscielny, Kieran Gibbs na Bacary Sagna. Mabeki hao wamekumbusha zama ambazo wa kina Dixon, Adams, Bould au Keown na Winterburn walikuwa wakiunda ukuta bora wa Arsenal uliofanya timu hiyo itambe katika Ligi Kuu ya Uingereza na kujizolea umaarufu mkubwa. Ukiangalia rekodi nzuri waliokuwa nayo Arsenal kwa kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 12 katika mechi 16 za mashindano yote msimu huu utaona ni kwanini klabu hiyo inaongoza ligi pamoja na kundi lao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment