Saturday, November 9, 2013

MAN CITY HAWAKUPASWA KUMUACHA HART - SCHMEICHEL.

GOLIKIPA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Peter Schmeichel amedai kuwa klabu ya Manchester City haikupaswa kumuacha golikipa namba wa Uingereza Joe Hart kwasababu nyota huyo ana kipaji cha kipekee. Hart alipoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha City na kurithiwa na Costel Pantilimon baada ya kufanya makosa yalioigharimu klabu hiyo. Lakini Schmeichel ambaye amecheza katika vilabu vyote hivyo vya Manchester anadhani Hart hajafanya makosa mpaka kusababisha kuachwa. Schmeichel amesema kuna kipindi mambo hayawezi kwenda sawa lakini kwa jinsi inavyoonekana kwa Hart ni kama kaua mtu wakati ni makosa ya kawaida katika mchezo.

No comments:

Post a Comment