Saturday, November 9, 2013

RONALDO ANAPATA MOTISHA KUTOKA KWA MESSI - PIGUE.

BEKI mahiri wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique amedai kuwa Cristiano Ronaldo anapata motisha kutoka kwa hasimu wake Lionel Messi hatua inayopelekea awe katika kiwango chake cha juu. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amekuwa akimaliza kama mshindi wa pili katika tuzo za Ballo d’Or katika kipindi cha miaka miwili iliyopita huku mwaka huu pia wakiwa katika kinyang’anyiro hicho. Pique ambaye alicheza kwa kipindi kifupi Manchester United anafikiri Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 anapata nguvu za kujituma zaidi kutoka kwa Messi na kumsifu nyota huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno kwa juhudi zake hizo. Pique amesema Ronaldo hajabadilika toka wakiwa wote United, ni mchezaji ambaye anamuhusudu kwasababu anafanya kazi kwa bidii kuwepo hapo alipo.

No comments:

Post a Comment