Saturday, November 9, 2013

NI HESHIMA KUWA MWEUSI PEKEE KATIKA TUZO ZA BALLON D'OR.

KIUNGO wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure amesema ni heshima kubwa kwake kuwa Mwafrika pekee kuteuliwa kugombea tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama FIFA Ballon d’Or. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye anashikilia tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika anajivunia kujulikana kama mmoja wa wachezaji bora duniani na ndio sababu anajituma kwa bidii zaidi. Toure amesema kuna wachezaji wengi wazuri na wenye vipaji barani Afrika lakini kitendo cha yeye kuonekana na kuwekwa katika orodha hizo ni heshima kubwa nay a kipekee kwake. Toure alikuwa jijini Nairobi Kenya wiki iliyopita kama balozi wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa-UNEP wakati majina ya watakaogombea tuzo hiyo yalipotajwa.

No comments:

Post a Comment