Saturday, November 9, 2013

TIMU TANO NDIO ZIKO KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA LIGUE 1 - BLANC

KOCHA wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Laurent Blanc anaamini kuwa kuna timu tano ndio zenye uwezo wa kugombe taji la Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1. PSG kwasasa ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na alama 28 katika mechi 12 walizocheza, wakifuatiwa na Lille na Monaco walioko katika nafasi ya pili na tatu huku wakiwa wametofautiana kwa kwa alama mbili pekee. Blanc amesema Lille wanaoenakana washindani katika mbio za ubingwa katika ligi hiyo pamoja na kwamba vyombo vya habari vinatoa nafasi kubwa kwa timu mbili ambazo ni PSG na Monaco. Mbali na Lille pia ziko timu kama Nantes na Olympique Marseille nazo pia zina nafasi hiyo kwasababu hawajatofautiana kwa alama nyingi.

No comments:

Post a Comment