Sunday, November 10, 2013

RONALDO ANATOKEA SAYARI NYINGINE - ANCELOTTI.

KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amemuelezea Cristiano Ronaldo kama mchezaji mwenye kipaji kutoka katika sayari nyingine tofauti na hii baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kutupia mabao matatu katika ushindi wa mabao 5-1 waliopata dhidi ya Real Sociedad jana. Mabao ya Ronaldo yanamfanya kufikisha mabao 24 katika mechi 17 alizocheza msimu huu wakati Madrid wakiwakaribia vinara Barcelona katika msimamo wa La Liga. Akihojiwa Ancelotti amesema Ronaldo ana kiwango cha sayari nyingine hakuna maelezo mengine unayoweza kusema zaidi ya hayo. Ancelotti aliendelea kudai kuwa nyota huyo amekuwa akifunga suala la ufungaji kuonekana kama ni rahisi hivyo ni ngumu kumfananisha.

No comments:

Post a Comment