Sunday, November 10, 2013

WE CAN MATCH 1992 MANCHESTER UNITED - WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anaamini kuwa msingi wa wachezaji vijana alionao unaweza kuleta mafanikio kama vijana wa darasa la mwaka 1992 wa timu ya Manchester United. Arsenal itakuwa mgeni wa United katika Uwanja wa Old Traford katika mchezo wa Ligi ya Kuu ya Uingereza baadae leo. Wenger amesema United walikuwa na kikosi cha kipekee kipindi hicho ambacho kilijumuisha nyota kama Gary Neville, Phil Neville, David Beckham, Ryan Giggs, Paul Scholes na Nicky Butty. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kundi alilonalo hivi sasa linaweza kuleta mafanikio kama ilivyokuwa kwa kundi hilo la United.

No comments:

Post a Comment