Sunday, November 10, 2013

MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA 2022 YA QATAR HAIWEZI KUINGILIANA NA WINTER OLIMPIKI - BLATTER.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amedai kuwa michuano ya Kombe ya Dunia itakayofanyika nchini Qatar haitachezwa katika kipindi cha mwezi Januari au Februari mwaka 2022 kwasababu ya michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi. Blatter amesema badala yake michuano hiyo inaweza kuhamishwa na kuchezwa katika kipindi cha Novemba au Desemba mwaka huo. FIFA inataka kuhamisha michuano hiyo kutokana na hofu ya joto kali linalofikia nyuzi joto zaidi ya 40 katika kipindi cha kiangazi hatua ambayo inaweza kuwaweka wachezaji na mashabiki katika hatari. Blatter amesema haitawezekana michuano miwili tofauti kuchezwa kwa wakati mmoja hivyo kuna uwezekani Kombe la Dunia 2022 kuchezwa mwishoni mwa mwaka huo. Blatter amesema kuipeleka michuano hiyo mwaka 2023 itakuwa ni kuikosea heshima michuano ya olimpiki na pia kwasababu wanatumia vyombo hivyo hivyo vya habari, luninga na wadau wa masoko wanaofanana.


No comments:

Post a Comment