Sunday, November 10, 2013

USHINDI DHIDI YA DORTMUND NI MUHIMU KATIKA KUTETEA UBINGWA WETU - RIBERY.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery amedai kuwa ushindi watakaopata katika mchezo wao nyumbani kwa Borussia Dortmund utawaweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao la Bundesliga. Mabao yaliyofungwa na Jerome Boateng, Ribery na Thomas Muller yalitosha kuisadia timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Augsburg jana hivyo kuongeza idadi ya mechi ambazo hawajafungwa msimu huu kufikia 37. Pamoja na kufurahia ushindi huo Ribery aliwakumbuka mahasimu wao Dortmund ambao wanakutana Novemba 23 na kudai kuwa mchezo huo utakuwa ni muhimu kwao katika mbio zao za kutetea taji lao. Kocha wa Bayern Pep Guardiola naye amewaonya wachezaji wake kwamba wanatakiwa kuongeza bidii pamoja na ushindi huo waliopata kwasababu hawakucheza vyema. Guardiola amesema ilikuwa vizuri kupata bao la kuongoza mapema lakini baada ya hapo hawakucheza vizuri mpaka katika kipindi cha pili walivyoweza kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi.

No comments:

Post a Comment