Sunday, November 3, 2013

ERIKSSON ADAI KUSAINI MKATABA NA MANCHESTER UNITED.

MENEJA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Sven Goran Eriksson amedai kuwa alisaini mkataba kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson katika klabu ya Manchester United mwaka 2002. Ferguson alikuwa amepanga kustaafu mwaka huo na Eriksson alidai kufutwa na maofisa wa United kwa ajili ya kuchukua nafasi yake na hata kufikia hatua ya kusaini mkataba. Eriksson ambaye ni raia wa Sweden alikuwa amepanga kuitema Uingereza lakini Ferguson alibadili mawazo na kuendelea kubakia Old Traford kwa muongo mwingine mmoja wakati Eriksson yeye aliacha kuinoa Uingereza mwaka 2006. Eriksson alibainisha hayo katika kitabu chake kipya kilichotoka hivi karibuni kikielezea kwa undani maisha yake ya ukocha katika nchi na vilabu mbalimbali alivyofundisha.

No comments:

Post a Comment