Monday, November 4, 2013

VETTEL AZIDI KUWATESA KATIKA LANGALANGA.

DEREVA wa Red Bull, Sebastian Vettel ameendelea kutesa kwenye mbio za magari za Langalanga baada ya kushinda kwenye mashindano ya Grand Prix ya Abu Dhabi na kufanya kuwa ushindi wake wa saba mfululizo. Vettel,ambaye tayari amevikwa taji la dunia aliongoza kwenye kila mzunguko na kufanikiwa kumshinda dereva mwenzake wa Red bull Mark Webber, dereva wa Mercedes Nico Rosberg na yule wa Lotus Romain Grosjean. Dereva wa Ferrari Fernando Alonso alikamata nafasi ya tano katika mbio hizo huku aul Di Resta wa Force India na Lewis Hamilton wakishika nafasi ya sita na saba. Akihojiwa mara baada yam bio hizo Vettel alishukuru mashabiki na watu wote walioko nyuma yake wakimsaidia kwa kumaliza mwaka akiwa katika nafasi ya juu.

No comments:

Post a Comment