Monday, November 4, 2013

IBRAHIMOVIC ASINGENISUMBUA - KLOPP.

KOCHA wa timu ya Borussia Dortmund Jurgen Klopp anaamini kuwa angeelewana vyema na mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic kama angefanya nae kazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden anajulikana kama mmoja wa wachezaji wenye vipaji na wakorofi lakini Klopp ana uhakika asingepata shida kufanya nae kazi. Klopp amesema wangeishi vizuri kwasababu wachezaji watukutu kama Ibrahimovic huwa wanampenda nay eye hajui kwanini. Pamoja na kauli hiyo ya Klopp, navyonekana wawili pengine hawataweza kufanya kazi pamoja kutokana na kusaini mikataba mipya katika vilabu vyao. Klopp amesaini mkataba na Dortmund unaomalizika 2018 wakati Ibrahimovic amesaini mkataba na SG unaomalizika 2016.

No comments:

Post a Comment