Monday, November 4, 2013

NADAL, DJOKOVIC KUGOMBEA NAFASI YA KWANZA LONDON.

WACHEZAJI nyota wa tenisi Rafael Nadal wa Hispania na Novak Djokovic wa Serbia watajitupa uwanjani katika msimu wa mwisho wa michuano ya ATP World Tour itakayofanyika London michuano ambayo itaamua nani atamaliza msimu katika nafasi ya kwanza. Djokovic anayeshika nafasi ya pili katika orodha za ubora duniani alifufua matumaini ya kurejea katika nafasi ya kwanza aliyopokwa na Nadal baada ya kushinda michuano ya Paris Masters jana. Nyota hao wote wawili wataanza kutupa karata zao kesho katika mechi zitakazofanyika katika Uwanja wa O2 Arena. Nadal atakwaana na Mhispania mwenzake David Ferrer katika mchezo wa kwanza wakati bingwa mtetezi wa michuano hiyo Djokovic atakwaanza na Roder Federer wa Switzerland.

No comments:

Post a Comment