Wednesday, November 13, 2013

FIFA KUTUMIA MAABARA YA USWIS ILI KUPIMA SAMPULI ZA MKOJO NA DAMU KATIKA KOMBE LA DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka Dunia-FIFA limeamua kutumia maabara ya nchini Switzerland kupima sampuli za mkojo na damu kwa wachezaji kwenye michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil mwakani. Brazil ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo iakayochezwa katika kipindi cha majira kiangazi mwakani hawana maabara iliyokamilika kwa ajili ya kutambua wanaotumia dawa za kusisimua misuli. Mapema mwaka huu Shirika la Kupambana na Dawa hizo Duniani - WADA ilipinga hadhi ya maabara iliyopo jijini Rio de Janeiro kutumika katika michuano hiyo. Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuwa uamuzi waliochukua haukuwa wao peke yao bali walishirikiana na WADA ili kuhakikisha wanapata mahala sahihi kwa ajili ya shughuli hiyo.

No comments:

Post a Comment