Wednesday, November 13, 2013

AL AHLY YAAMUA KUMUUZA ABDUL ZAHER.

KLABU ya Al Ahly ya Misri imetangaza kumuweka sokoni mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Ahmed Abdul Zaher kufuatia ishara yenye utata aliyoonyesha wakati wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika Jumamosi iliyopita. Baada ya kufunga bao katika mchezo huo ambao uliisha kwa Al Ahly kushinda kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Orlando Pirates, Zaher alipiga saluti ya vidole vinne ishara ambayo hutumiwa na waandamanaji wanaomuunga mkono rais aliyeondolewa Mohamed Morsi. Maandamano ya watu hao yalipelekea vifo vya mamia ya watu. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, mbali na nyota huyo kuwekwa sokoni lakini pia ameenguliwa katika kikosi cha timu hiyo ambacho kitashiriki michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia itakayofanyika nchini Morocco Desemba mwaka huu. Taarifa hiyo imesema imeamua kutoa adhabu hiyo kwasababu sababu za kikanuni ambazo zinakataza kuchanganya mchezo wa soka na mambo ya siasa.

No comments:

Post a Comment