Wednesday, November 13, 2013

APOTEZA NYUMBA KWA KUCHEZA KAMARI UGANDA.

SHABIKI mmoja wa klabu ya Arsenal katika Wilaya ya Iganga Kaskazini mwa Uganda anatafuta nyumba nyingine kwa ajili ya familia yake baada ya kupoteza nyumba aliyokuwa akiishi katika kamari kwenye mechi kati ya timu ya Arsenal na Manchester United. Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti la Obsever la nchi hiyo, zimedai kuwa kabla ya mchezo baina ya timu hizo za Uingereza Jumapili iliyopita, Henry Dhabasani aliweka rehani nyumba yake ya vyumba viwili na Rashidi Yiga kwamba Arsenal wangeshinda mchezo huo. Kwa upande wa Yiga yeye aliweka rehani gari lake jipya aina ya Toyota Premio pamoja na mkewe kwamba Manchester United wangeshinda mchezo huo. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa wawili hao waliweka dau lao katika maandishi huku viongozi wa eneo hilo pamoja na mashabiki wakishuhudia tukio hilo. Dhabasani ambaye ana wake watatu na watoto watano, alizimia mwishoni mwa mechi hiyo baada ya Arsenal kufungwa kwa bao 1-0, ambapo siku ya Jumatatu mashabiki wa United walivamia nyumbani kwake na kumtimua katika nyumba hiyo aliyoiweka rehani.

No comments:

Post a Comment