Wednesday, November 13, 2013

ARSENAL YAFIKIRIA KUMUONGEZA MKATABA ROSICKY.

KLABU ya Arsenal imepanga kumuongeza Thomas Rosicky mkataba wa mwaka mmoja zaidi kama akifanikiwa kucheza mechi 25 kwa timu hiyo msimu huu. Mkataba wa sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 unatarajiwa kuisha mwishoni kipindi cha majira ya kiangazi mwakani. Rosicky alijiunga na Arsenal akitokea klabu ya Borussia Dortmund mwaka 2006, ambapo msimu huu amecheza mechi 11 huku nane kati ya hizo akianza katika kikosi cha kwanza ikiwemo mechi dhidi ya Liverpool na Dortmund. Nyota huyo wa Jamhuri ya Czech siku zote amekuwa akipewa nafasi na Wenger pamoja na kutumia muda wake mwingi akiwa majeruhi.

No comments:

Post a Comment