Wednesday, November 13, 2013

GERRARD, WALKER KUIKOSA CHILE.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Steven Gerrard na beki Kyle Walker wanatarajiwa kukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Chile utakaofanyika katika Uwanja wa Wembley. Gerrard ambaye anakipiga katika klabu ya Liverpool alipata majeraha wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Fulham mwishoni mwa wiki wakati Walker anayekipiga katika timu ya Tottenham Hotspurs nae alikosa kufanya mazoezi na wenzake. Mbali na hao nyota wengine watakaokosa mechi hiyo ni pamoja na Michael Carrick na Danny Wilbeck walioondolewa jana. Uingereza itakwaana na Chile Ijumaa na baadae kuikaribisha Ujerumani siku nne baadae.


No comments:

Post a Comment