Tuesday, November 12, 2013

FIFA YABADILI WAAMUZI MECHI YA NIGERIA NA ETHIOPIA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limebadilisha waamuzi watakaochezesha mechi ya mkondo wa pili ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 kati ya wenyeji Nigeria na Ethiopia itakayofanyika jijini Calabar. Mwamuzi wa Kenya Aden Marwa Range nafasi yake itachukuliwa na Felicien Kabanda ambaye ameteuliwa kuwa mwamuzi msaidizi namba mbili katika mchezo huo. Mwamuzi mwenye uzoefu Bakary papa Gassama wa Gambia mwenye umri wa miaka 34 ndio atakuwa mwamuzi kati katika pambano hilo wakati Angeson Agbamariam atakuwa mwamuzi msaidizi wa kwanza na Maudo Jallow akiwa kama kamisaa. Nigeria itacheza na Ethiopia Novemba 19 mwaka huu katika mchezo wa pili huku wakiwa mbele baada ya kushinda kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza.


No comments:

Post a Comment