MSHAMBULIAJI mkongwe wa klabu ya Al Ahly Mohamed Abu Trika hakupokea medali yake ya ushindi wakati timu yake iliponyakuwa taji la michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini. Toka kutokea tukio hilo vyombo vya habari vya Misri vimekuwa vikijadili kama mkongwe huyo atapewa adhabu yoyote kutoka na hilo. Abu Trika mwenye umri wa miaka 35 aliiongoza Al Ahly kushinda taji lake la nane la michuano hiyo baada ya kufunga mabao katika mechi za mikondo yote miwili yaani Afrika Kusini na Cairo. Kumekuwa na tetesi zilizozagaa kuwa nyota huyo hakuongozana na wenzake kwenda kuchukua medali kutoka kwa Waziri wa Michezo kwasababu ya msimamo wake na serikali ya sasa ya Misri. Waziri wa michezo Taher Abu Zaied amesema anasubiri maelezo ya nyota huyo kabla hajaamua kufanya chochote.
No comments:
Post a Comment