Tuesday, November 12, 2013

MESSI NJE MIEZI MIWILI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha kati ya wiki sita na nane kwasababu ya majeraha ya msuli wa nyuma ya paja yanayomsumbua. Messi mwenye umri wa miaka 26 alitolewa katika kipindi cha kwanza Jumapili iliyopita katika mchezo dhidi ya Real Betis na iligundulika kuwa alichanika msuli wa paja katika mguu wake wa kushoto. Msimu huu umekuwa sio mzuri kwa nyota huyo kutokana na majehara ya mara kwa mara yanayoamuandama kuanzia Septemba mwaka huu. Katika taarifa zilizotumwa katika mtandao wa Barcelona zimedai kuwa hatua ya kwanza ya matibabu ya nyota huyo itafanyika hapohapo chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo na baadae atasafiri kwenda jiji Buenos Aires kwa mapumziko zaidi.

No comments:

Post a Comment