Tuesday, November 12, 2013

DJOKOVIC AELEKEZA NGUVU ZAKE BILGRADE.

Novak Djokovic ameendelea kutesa katika mashindano ya dunia ya ATP baada ya kufanikiwa kulitetea akimshinda mchezaji anayeongoza kwa ubora duniani Rafael Nadal. MSerbia huyo ambaye alipoteza nafasi yake ya kwanza kwa Nadal mwezi uliopita, alishinda kwa mchezo wake aliokutana na Nadal 6-3 6-4 katika mchezo uliofanyika katika wa O2 Arena jijini London. Djokovic mwenye umri wa miaka 26, sasa anafikisha michezo 22 kucheza bila kufungwa na taji hilo la mwishoni mwa msimu linakuwa ni la tatu kwake. Nyota huyo sasa nguvu zake anazielekeza huko Belgrade, ambako timu ya Serbia itacheza na Czech Republic katika michuano ya Davis Cup Ijumaa.


No comments:

Post a Comment