Monday, November 11, 2013

MESSI ANAHITAJI MUDA WA KUPUMZIKA ILI APONE VIZURI - FABREGAS.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Cesc Fabregas amedai kuwa mchezaji mwenzake Lionel Messi anahitaji kuchukua muda wa kupumzika kucheza soka ili kuruhusu mwili wake kupona kufuatia majeraha yanayomsumbua. Messi mwenye umri wa miaka 26 alitolewa nje kati kati ya kipindi cha kwanza katika mechi dhidi ya Real Betis ambayo Barcelona ilishinda kwa mabao 4-1 na kupelekea nyota huyo wa kimataifa wa Argentina kucheza mechi tano za La Liga bila kufunga. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Fabregas amesema Messi anahitaji kupumzika ili kuupa muda mwili wake uweze kurejea katika hali yake ya kawaida kutokana na mikiki mikiki ya kipindi kirefu. Fabregas aliendelea kudai kuwa yeye pia alikuwa anasumbuliwa na tatizo kama la Messi, kwani unaweza kukaa kwa kipindi kifupi ukadhani umepona kumbe bado na ukirejea uwanjani unajitonesha tena.

No comments:

Post a Comment