Monday, November 11, 2013

GOODLUCK JONATHAN AWAJAZA VIJANA MAPESA BAADA UA KUNYAKUA KOMBE LA DUNIA.

RAIS wa Nigeria, Goodluck Jonathan ametangaza zawadi ya fedha kwa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka ya nchi hiyo kufuatia kunyakuwa Kombe la Dunia la vijana wa umri wa huo huko Falme za Kiarabu-UAE. Jonathan ambaye aliwakaribisha vijana hao katika tafrija aliyoiandaa ikulu jijini Abuja amewapa kila mchezaji dola 12,626 sawa na naira milioni mbili na kocha mkuu Manu Garba amepewa kitita cha dola 18,939 sawa na naira milioni tatu. Makocha wasaidizi wa kikosi hicho Emmanuel Amuneke, Nduka Ugbade na Emeka Amadi kila mmoja amelamba kiasi cha dola 15,782 sawa naira milioni mbili na nusu wakati wajumbe wengine wa benchi la ufundi wamepatiwa kiasi cha kati ya dola 1,000 mpaka 3,000. Nigeria walinyakua taji hilo baada ya kuwachapa Mexico kwa mabao 3-0 Ijumaa iliyopita hilo likiwa taji la nne la dunia kwa nchi hiyo huku yote wakiwa wamenyakuwa katika ardhi ya bara la Asia. Nigeria wamewahi kunywakua taji hilo katika michuano ya mwaka 1985 iliyofanyika China, Japan mwaka 1993, Korea Kusini mwaka 2007 na sasa UAE.

No comments:

Post a Comment