Monday, November 11, 2013

RONALDO AKINYEMELEA KIATU CHA DHAHABU ULAYA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameendelea kuongoza katika orodha ya kinyang’anyiro cha tuzo ya Ulaya ya Kiatu cha Dhahabu kufuatia kuonyesha kiwango bora katika mchezo dhidi ya Real Sociedad mwishoni mwa wiki iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alifunga mabao matatu na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Sociedad na kufikisha mabao 16 katika msimu wa 2013-2014. Nafasi ya pili katika orodha hizo inashikiliwa na Nerijus Valski wa klabu ya Suduva ya Lithuania huku Diego Coasta wa Atletico Madrid akiwa katika nafasi tatu. Nyota hao wote wamekaa katika nafasi hizo baada ya kufanya vyema katika vilabu vyao katika mechi za mwishoni wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment