Friday, November 1, 2013

RAIS WA NIGERIA AMTUMIA MWALIKO BINAFSI ABU TRIKA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa zamani wa Misri na klabu ya Al Ahly Mohamed Abu Trika amepokea mwaliko kutoka Shirikisho la Soka la Nigeria-NFF kucheza mchezo wa kirafiki kwa ajili ya wahanga wa saratani Desemba mosi mwaka huu. Al Ahly ilitangaza kuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alimpa mwaliko binafsi veterani huyo katika soka. Kwa upande mwingine Al Ahly wamebainisha kuwa hawatamzuia nyota huyo kusafiri kwenda Nigeria kama timu itakuwa haina ratiba yoyote katika kipindi hicho. Abu Trika kwasasa yupo na timu hiyo nchini Afrika Kusini wakati wakijiandaa na fainali ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates itakayochezwa Jumamosi.

No comments:

Post a Comment