Friday, November 1, 2013

ROMA YAWEKA REKODI SERIE A.

KLABU ya AS Roma imekuwa timu ya kwanza kushinda mechi zao 10 za kwanza za Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A baada ya kuifunga Chievo kwa bao 1-0 jana. Katika mchezo huo Roma walijipaia bao lao la ushindi katika dakika za majeruhi kwa mpira wa kichwa uliopigwa na Marco Boriello. Roma chini ya kocha mpya Rudi Garcia aliyeanza kuinoa timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu, imefikisha alama 30 katika msimamo wa Serie A, ikiwa ni alama tano zaidi ya Juventus na Napoli zinazoshika nafasi ya pili na tatu. Roma inakabiliwa na mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Torino Jumapili.

No comments:

Post a Comment