Friday, November 1, 2013

NADAL, DJOKOVIC WATISHA MICHUANO YA PARIS MASTERS.

MCHEZAJI nyota tenisi anayeshika namba moja kwa ubora dunia, Rafael Nadal na Novak Djokovic anayeshika namba mbili, wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Paris Masters baada ya kushinda mechi zao za mzunguko wan ne. Nadal alimgaragaza Jerzy Janowicz kwa seti 2-0 zenye alama za 7-5 6-4 wakati Djokovic alimtandika John Isner kwa seti 2-1 zenye alama za 6-7 6-1 6-2. Kwa upande mwingine Roger Federer naye alijihakikishia nafasi hiyo kwa kumchapa Philipp Kohlschreiber kwa 6-3 6-4 ambapo sasa atakwaana na Juan Martin Del Porto katika hatua ya robo fainali.
David Ferrer, Del Porto na Thomas Berdych wataungana na Federer, Djokovic na Nadal katika msimu wa mwisho wa michuano ya ATP Tour jijini London mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Paris Masters.

No comments:

Post a Comment