SERIKALI ya Brazil imesema itaongeza ndege pamoja na kuzindua njia mpya ili kukabiliana na foleni kubwa kwenye usafiri wa anga itakayokuwepo wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Waziri anayeshughulika na masuala ya usafiri wa anga, Wellington Moreira Franco amesema serikali imepanga kuongeza ndege katika njia zilizopo na kufungua njia zingine mpya ili kupunguza msongamo wakati wa michuano hiyo. Kauli ya serikali imekuja kufuatia kilio cha wananchi waliokuwa wakilalamikia nauli kubwa ya usafiri wa anga katika michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza toka mwaka 1950. Tayari serikali ya Brazil imesikia kilio hicho na kukutana na wawakilishi wa mashirika ya ndege nchini ili kujadili utaratibu wa nauli inayoeleweka wakati wa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment