Thursday, October 31, 2013

TOTTENHAM WALICHEMKA KUNISAJILI - PATO.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Corinthians Alexandre Pato amethibitisha kuwa Tottenham Hotspurs walishindwa ofa yao ya kutaka kumsajili katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi. Akihojiwa kuhisiana na hilo Pato amesema Tottenham waliwasiliana na Corinthians kuhusu uhamisho wake lakini yeye na wakala wake waliamua kuwa anahitaji kubakia hapo. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil aliibukia barani Ulaya wakati akiwa na umri wa miaka 17 mwaka 2007 wakati alipoifungia bao timu yake ya AC Milan katika mchezo wa Serie A dhidi ya Napoli. Pato alifanya vyema katika msimu wa 2010-2011 wakati alipoifungia Milan mabao 14 lakini aliporomoka ghafla baada ya kuanza kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara yaliyopelekea kuamua kurejea nchini kwao Brazil.


No comments:

Post a Comment