Monday, November 18, 2013

VETTEL AVUNJA REKODI KATIKA LANGALANGA.

DEREVA mahiri wa mashindano ya langalanga wa timu ta Red Bull, Sebastian Vettel ameweka rekodi mpya ya kushinda mfululizo kwa msimu mmoja baada ya kuibuka kidedea katika mashindano ya Grand Prix ya Marekani. Kwa ushindi huo Vettel anakuwa ameshinda mashindano nane mfululizo na kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Michael Schumacher na Alberto Ascari. Dereva wa Lotus Romain Grosjean alishika nafasi ya pili mbele ya Mark Webber pia wa Red Bull aliyeshika nafasi ya tatu. Lewis Hamilton wa Marcedes alishika nafasi ya nne akiwashinda Fernando Alonso wa Ferrari na Nico Hulkenberg wa Sauber walioshika nafasi ya tano na sita.

No comments:

Post a Comment