MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa kimataifa wa Misri Mohamed Abou Trika anatarajia kuandika historia mpya katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia kabla ta kustaafu rasmi mchezo wa soka. Aboutrika mwenye umri wa miaka 35 alitangaza kutundika daruga mara baada ya michuano hiyo ambayo inafanyika nchini Morocco. Mkongwe huyo anaweza kuweka rekodi ya kufunga mabao manne katika michuano hiyo na kufikia rekodi ya mshambuliaji nyota wa Argentina Lionel Messi na Denilson wa Brazil wakati timu yake ya Al Ahly itakapokwaana na Guangzhou Evergrade ya China jijini Agadir baadae leo. Katika mchezo huo Al Ahly ndio wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na uzoefu wao katika michuano hiyo ambapo wamewahi kushika nafasi ya tatu mwaka 2006 katika michuano iliyofanyika nchini Japan huku wakitinga robo fainali mwaka jana.
No comments:
Post a Comment