Friday, December 13, 2013

FA KUFIKIRIA OMBI LA HULL CITY KUBADILI JINA.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza, FA, kitashauriana na mashabiki kabla ya kufikiria ombi ya kubadilisha jina liliwasilishwa na klabu ya Hull City. Hatua hiyo imekuja kufuatia mmiliki wa klabu hiyo Assem Allam kutuma maombi rasmi kwa FA kuomba kubadilisha jina la timu hiyo kuitwa Hull Tigers badala ya Hull City. Katika taarifa yake FA imedai kuwa itashauriana na wanahisa mbalimbali wa klabu hiyo ikiwemo makundi ya mashabiki. Baadhi ya makundi ya mashabiki wa klabu hiyo wana uhakika kuwa FA itachukua uamuzi sahihi kuhusiana na suala hilo Mashabiki wa klabu hiyo wanapinga jina lake kubadilishwa na kuitaka FA kulinda urithi na utamaduni wa michezo.

No comments:

Post a Comment