KLABU ya Barcelona imethibitisha kuwa inapanga kujenga uwanja mwingine wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 105,000 ambao utakuwa uwanjani wa tatu kwa ukubwa duniani. Msemaji wa klabu hiyo Toni Freixa amesema kuwa wanatarajia kupiga kura ya maoni mwakani kama waufanyie ukarabati uwanja wa sasa wa camp Nou ili kuuongeza ukubwa au watafute eneo la karibu na mji huo ili kujenga uwanja mpya. Kama mpango huo ukikamilika uwanja huo mpya utakuwa ni wa tatu kwa kuingiza idadi kubwa ya mashabiki ukitanguliwa na Uwanja wa Rungrado May Day uliopo Korea Kaskazini wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 150,000 na Uwanja wa Saltlake uliopo Calcuta wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 120,000. Uwanja unaotumiwa hivi sasa na Barcelona una uwezo wa kuingiza mashabiki 99.354.
No comments:
Post a Comment