SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limedai kuwa uamuzi wa kama watahamisha tarehe ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 utaamuliwa Desemba mwakani. Rais FIFA Sepp Blatter alitangaza Octoba kuwa wameteua kikosi kazi cha kuangalia tarehe itakayokuwa muafaka kwa ajili ya michuano hiyo. Hatua hiyo imekuja kufuatia wasiwasi wa joto kali linaloweza kufikia nyuzi joto 50 katika majira ya kiangazi ambayo ndio michuano hiyo huchezwa. Waandaaji wa michuano hiyo nchini Qatar wamesema wana uwezo wa kuandaa muchuano hiyo katika muda wowote katika mwaka lakini kamati hiyo imedai kuwa itasikiliza lolote litakaloamualiwa na viongozi hao.
No comments:
Post a Comment