Friday, December 6, 2013

MBWANA SAMATTA ASHINDWA KUPENYA ORODHA ZA CAF.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetangaza orodha ya mwisho ya wachezaji watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wanaocheza nje na ndani ya Afrika huku mshammbuliaji nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta akishindwa kupenya katika orodha hiyo. Samatta anayecheza katika klabu ya TP mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC alikuwepo katika orodha ya kwanza iliyowahusisha jumla ya wachezaji 21 kutoka pembe mbalimbali barani Afrika. Katika hao wote ni wachezaji watano pekee waliopenya katika orodha ya wachezaji watakaogombea tuzo hiyo kwa wachezaji wanaocheza soka barani Afrika na wengine 10 wanaochezaji soka ya kulipwa barani Ulaya na kwingineko. Wachezaji hao waliopenya katika orodha hiyo watapigiwa kura na makocha kutoka vyama vya michezo ambavyo ni wajumbe wa CAF ili kupata mshindi wa vipengele hivyo viwili. Wachezaji waliopenya katika kipengele cha kwanza cha wachezaji wanaocheza soka ya kulipwa nje ya Afrika ni pamoja na Yaya Toure na Didier Drogba wa Ivory Coast, Mohamed Abou Trika-Misri, John Obi-Mikel, Emmanuel Eminike, Ahmed Musa na Vincent Enyeama wa Nigeria, Asamoah Gyan-Ghana, Jonathan Pitroipa-Burkina Faso na Pierre-Emerick Aubameyang-Gabon. Orodha ya wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika ni pamoja na Mohamed Abou Trika-Misri, Tresor Mputu-DRC, Ahmed Fathy-Misri, Rainford Kalaba-Zambia na Sunday Mba-Nigeria

No comments:

Post a Comment