Friday, December 6, 2013

MSHINDI WA KOMBE LA DUNIA 2014 KUNYAKUWA KITITA CHA DOLA MILIONI 35.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza zawadi wa dola milioni 35 kwa mshindi atakayenyakuwa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke pia alitaja zawadi ya mshindi wa pili katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 12 kuwa itakuwa dola milioni 25. Zawadi hiyo imeongezwa ikilinganishwa na mwaka 2010 ambapo Hispania waliokuwa mabingwa wa michuano hiyo walinyakuwa kitita cha dola milioni 31. Timu itakayomaliza katika nafasi ya tatu itanyakuwa kitita cha dola milioni 22 huku mshindi wa akiondoka na dola milioni 20 wakati timu zitakazofanikiwa kutinga hatua ya mtoano zitapata uhakika wa kuondoka na dola milioni nane kila moja.

No comments:

Post a Comment