KOCHA wa klabu ya Barcelona, Gerardo Martino amesema hana uhakika kama Lionel Messi atakuwa fiti na kuwepo katika kikosi chake mara watakaporejea kutoka katika mapumziko mafupi ya majira ya baridi Januari mwakani. Messi atakuwa nje ya uwanja kwa mwaka wote huu uliobakia baada ya kuchanyika msuli wa nyuma ya paja mwezi uliopita na kutokuwepo kwake kumeshuhudia Barcelona ikipoteza michezo miwili mfululizo kwa mara ya kwanza toka Machi mwaka huu. Barcelona ambayo ilikuwa haijafungwa toka masimu mpya wa Ligi Kuu nchini Hispania uanze, ilijikuta ikipoteza mchezo mbele ya Atletico Bilbao mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni siku tano toka timu hiyo ilipofungwa na Ajax Amsterdam kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Messi kwasasa amerejea nchini kwao Argentina akiendelea kujiuguza na anategemewa kurejea Barcelona mwanzoni mwa Januari. Hata hivyo Martino alikataa kuthibitisha kama nyota huyo atakuwa fiti kwa ajili ya kurejea uwanjani mwanzoni mwa mwaka 2014 ambapo Barcelona watakuwa wageni wa Atletico Madrid Januari 12.
No comments:
Post a Comment