KOCHA Claude Le Roy raia wa Ufaransa ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Congo Brazaville. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 aliyekuwa akiinoa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo-DRC amepewa mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo. Le Roy anachukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mfaransa mwenzake kamel Djbour. Hii inakuwa nchi ya tano ya Afrika kwa kocha huyo baada ya kuzifundisha pia Cameroon ambayo aliiwezesha kushinda taji la Mataifa ya Afrika mwaka 1988, Senegal, DRC na Ghana. Le Roy pia amewahi kufanya kazi katika nchi za Malaysia, Oman na Syria.
No comments:
Post a Comment