Friday, December 6, 2013

SOKA LAOMBOLEZA KIFO CHA MADIBA.

WACHEZAJI, vilabu na viongozi mbalimbali wa soka wametumia mtandao wa kijamii wa twitter kuonyesha simanzi zao kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyefariki jana usiku. Wachezaji duniani kote walituma ujumbe katika kurasa zao za twitter kuelezea walivyoguswa na tukio hilo la kufariki Mandela aliyekuwa na umri wa miaka 95. Mandela alishuhudia fainali za kwanza za Kombe la Dunia zikiandaliwa katika ardhi ya Afrika na kuondoka kwake hakuna shaka kutaleta simanzi katika droo ya upangaji ratiba ya michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika baadae leo. Baadhi ya wachezaji na viongozi waliotuma salamu zao za rambirambi ni pamoja na Cristiano Ronaldo, Yaya Toure, Michael Carick, Emmanuel Adebayor, Sepp Blatter, Michel Platini, Lionel Messi, Vecent Kompany na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment