Thursday, December 5, 2013

FIFA YAOMBA "PO" KWA WANANCHI WA BRAZIL.

KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Valcke amewataka wananchi na wapenzi wa soka nchini Brazil kuunga mkono michuano ya Kombe la Dunia mwakani na kudai kuwa haitakuwa wakati muafaka kufanya maandamano. FIFA ina wasiwasi wa kupata upinzani kutoka kwa raia juu gharama na kuandaa mashindano hayo. Valcke amesema ni haki kuonyesha hisia na kwao ni muda muafaka lakini kwake anadhani huo sio muda muafaka. Valcke alifafanua kuwa kwake anaona sio muda muafaka kwasababu anadhani ni muda wa mashabiki wa soka wan chi hiyo kufurahia wakati huo wa kipekee ambao hawajaupata toka mwaka 1950. Waandamanaji wengi nchini humo wanaamini kuwa kuandaa michuano hiyo ni kupoteza fedha katika kipindi ambacho maisha yamekuwa magumu nchini humo.

No comments:

Post a Comment