Wednesday, December 4, 2013

KILI STARS YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUITANDIKA BURUNDI.

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Chalenji baada ya kuifunga Burundi 1-0 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi. Ushindi huo unaifanya Stars kufikisha alama saba baada ya kutoka sare mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zambia na baadae kuifunga Somalia kwa bao 1-0. Bao pekee la Stars katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji mahiri wa anaekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC Mbwana Samatta aliyefunga kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu. Kocha wa Stars Kim Poulsen aliamua kuwaanzisha wachezaji Samatta na Thomas Ulimwengu ambao haakuwemo katika mechi mbili za kwanza kwasababu ya majukumu ya klabu yao ya Mazembe.


No comments:

Post a Comment