Tuesday, December 3, 2013

KOSCIELNY HURU KUCHEZA KOMBE LA DUNIA.

BEKI wa kimataifa wa Ufaransa, Laurent Koscielny anaweza kuanza katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia baada ya kufungiwa mechi moja kutokana na kadi nyekundu aliyopata katika mchezo wa mtoano dhidi ya Ukraine. Msemaji wa FIFA aliliambia shirika la habari la AFP kuwa Koscielny alipewa adhabu hiyo ambayo tayari ameshaitumikia katika mchezo wa mkondo wa pili hatua ya mtoano ambapo Ufaransa ilishinda kwa jumla ya mabao 3-2. Beki huyo alipewa kadi nyekundu kwa vurugu mwishoni mwa mchezo wa mkondo wa kwanza ambao Ukraine iliifunga Ufaransa mabao 2-0 jijini Kiev na kulikuwa na wasiwasi kuwa angeweza kuongezewa adhabu zaidi itakayomfanya kushindwa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia. Hata hivyo taarifa hizo itakuwa ahueni kwa kocha Didier Deschamps ambaye sasa anaweza kumjumuisha beki huyo katika kikosi chake kitakachokwenda nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment