Tuesday, December 10, 2013

MASHABIKI ZAIDI MILIONI MOJA WATUMA MAOMBI YA TIKETI KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limesema zaidi ya mashabiki wa soka milioni 1.1 wametuma maombi ya tiketi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia itakayochezwa mwakani nchini Brazil katika saa 24 za kwanza baada ya mauzo ya tiketi hizo kufunguliwa. Dirisha hilo jipya la kuuza tiketi lililofunguliwa Jumapili iliyopita baada ya kufanyika kwa droo ya upangaji ratiba Ijumaa iliyopita linatarajiwa kufungwa Januari 30 mwakani. FIFA imedai kuwa kama idadi ya watu wanaohitaji tiketi hizo ikizidi kutafanyika kwa droo nyingine kwa mashabiki walioomba tiketi hizo. FIFA inatarajia kuuza tiketi milioni 3.3 kwa ajili ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment