MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amekiri kuwa ni kitu muhimu kwake kuweka rekodi mpya ya mabao katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amefunga bao lake la tisa katika mechi tano alizocheza katika ushindi dhidi ya Copenhagen jana mchezo ambao pia alikosa penati. Mbali na kufunga bao na kucheza katika cha juu, Ronaldo alionya kuwa bado hajarudi katika kiwango chake kufuatia majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua hivi karibuni. Ronaldo amesema timu imecheza vizuri na lengo lao limetimia, na ana furaha kuweka rekodi katika mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment