Monday, December 16, 2013

MURRAY, FERGUSON WANYAKUWA TUZO YA BBC.

MCHEZAJI nyota wa tenisi, Andy Murray amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya mwanamichezo wa bora wa mwaka 2013 inayoandaliwa na shirika la utangazaji la BBC. Murray raia wa Scotland alifanikiwa kuwa mwingereza wa kwanza katika kipindi cha miaka 77 kunyakuwa taji la michuano ya Wimbledon baada ya kumtandika Novak Djokovic katika mchezo wa fainali iliyochezwa katika majira ya kiangazi mwaka huu. Nyota huyo aliwashukuru mashabiki waliompigia kura kunyakuwa tuzo na kwa kumuunga mkono kwani wamemfanya ajiamini zaidi na kuwaahidi kutowaangusha. Mbali na Murray, lakini pia kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson naye alipewa tuzo hiyo kwa mafanikio aliyopata wakati akiinoa United pamoja na mchango wake katika soka kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment