MABINGWA wa Ulaya klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imetua nchini Morocco tayari kwa kushiriki michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia. Bayern ambao wameshinda taji la Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, wanashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza toka mfumo wa sasa wa kushirikisha mabingwa wa kila bara ulipozinduliwa mwaka 2005. Katika mfumo wa zamani ambao ulikuwa ukiitwa Kombe la Intercontinental ukishirikisha bingwa wa Ulaya na Amerika Kusini, Bayern waliwahi kushinda mara mbili mwaka 1976 kwa kuifunga Cruzeiro ya Brazil na mwaka 2001 walipoifunga Boca Juniors ya Argentina katika mchezo uliochezwa jijini Tokyo. Bayern watachuana na Guangzhou Evergrande ya China Kesho na kama wakifanikiwa kushinda mchezo huo watakwaana na aidha mabingwa wa Amerika Kusini Atletico Mineiro au wenyeji wa michuano hiyo Raja Casablanca katika mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi.
No comments:
Post a Comment