WACHEZAJI nyota wa klabu ya Galatasaray, Didier Drogba na Emmanuel Eboue wameepuka adhabu kutoka Shirikisho la Soka la Uturuki kwa kuonyesha fulana zenye maandishi ya kumkumbuka hayati Nelson Mandela wakati wa mchezo wa ligi. Baada ya kusikiliza kwa kifupi Kamati ya Nidhamu iliamua kutupilia malalamiko dhidi ya nyota hao wa kimataifa wa Ivory Coast yaliyowasilishwa na shirikisho hilo. Wachezaji wote wawili waliungwa mkono na klabu yao ambayo ilibandika bango kubwa lenye picha ya Mandela nje ya uwanja wao huku kukiwa na ujumbe uliosomeka “ Urithi wako uko katika mioyo yetu”. Shirikisho la Soka la Uturuki lilitishia kuwachukulia hatua wachezaji hao kwa madai kuwa ujumbe kuhusu kifo cha Mandela uliokuwa katika fulana zao ulikuwa na mahusiano ya mambo ya kisiasa kitu ambacho hakiruhisiwi wa mechi za soka.
No comments:
Post a Comment