NGULI wa soka wa Brazil, Ronaldo de Lima amempigia chapuo mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi kushinda taji la Ballon d’Or kwa mara ya tano mfululizo. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ameanguka mpaka watatu katika wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kunyakuwa tuzo hiyo akiwa nyuma ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na Franck Ribery wa Bayern Munich. Lakini Ronaldo ambaye amewahi kucheza katika klabu ya Barcelona na Madrid enzi zake amesema kuwa Messi anaweza kuchukua tuzo hiyo kwa mara nyingine huku akidai Muargentina huyo atakuja akiwa fiti zaidi kutokana na majeruhi yanayomsumbua hivi sasa. Ronaldo amesema Messi ametumia muda wa miaka iliyopita kucheza mechi nyingi sana hivyo majeraha yaliyompata sasa sio kitu kwani yanampa muda wa kupumzika. Ronaldo amewahi kushinda taji la Ballon d’Or mara mbili ambazo ni mwaka 1997 na 2002.
No comments:
Post a Comment